IQNA – Mamlaka za Ufaransa zimeanzisha uchunguzi kufuatia jaribio la kuchoma moto chumba cha kusalia cha Waislamu mjini Châtillon-sur-Seine, tukio ambalo maafisa wamelilaani kuwa ni kitendo cha kigaidi cha uoga na chenye chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3481095 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/16
IQNA – Mwanamke mchanga Muislamu aliyevaa hijaab ameshambuliwa na kutishiwa maisha ndani ya basi la jiji la Ottawa, Canada eneo la Kanata, katika tukio linalochunguzwa na polisi kama uhalifu unaochochewa na chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3481079 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/13
IQNA – Viongozi wa moja ya misikiti mikubwa zaidi nchini Australia wamesema wamepokea vitisho vya kuuwawa baada ya kutangazwa mpango wa kuweka vipaza sauti vipya kwa ajili ya adhana.
Habari ID: 3481059 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/09
IQNA-Australia imeingia katika kipindi kigumu cha chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia), hali iliyoibuka kwa kasi tangu kuanza kwa vita vya kikatili vya utawala wa Israel dhidi ya Gaza.
Habari ID: 3481020 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/30
IQNA – Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR) limeitaka kampuni ya uwekezaji ya Sequoia Capital kumwondoa mshirika wake Shaun Maguire, kufuatia chapisho la mitandao ya kijamii lililokosolewa vikali kwa kuendeleza chuki dhidi ya Waislamu.
Habari ID: 3480934 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/12
IQNA – Polisi nchini Uingereza wameanzisha uchunguzi kupitia kamera za usalama (CCTV) kufuatia tukio lililoripotiwa la matusi ya maneno dhidi ya waumini nje ya msikiti ulioko Haverhill, Suffolk.
Habari ID: 3480931 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/12
IQNA – Utafiti mpya umeonesha ongezeko la chuki na chuki dhidi Uislamu (Islamofobia) dhidi ya wahudumu wa afya Waislamu nchini Australia, hali inayowaathiri kisaikolojia kwa kiwango kikubwa.
Habari ID: 3480925 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/11
IQNA-Miaka ishirini baada ya mashambulizi ya 7/7 mjini London, Waislamu wa Uingereza bado wanahisi athari za kihisia na kijamii.
Habari ID: 3480910 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/07
IQNA – Mwanamke Muislamu alishambuliwa kwa ukatili mahali pake pa kazi huko Oshawa, Ontario, Canada katika tukio ambalo viongozi wa jamii wanaitaka polisi kulichunguza kama jinai ya chuki.
Habari ID: 3480893 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/04
IQNA – Mamlaka za Ufaransa zimeripoti ongezeko la asilimia 75 la matukio ya chuki dhidi ya Waislamu katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2025, huku mashambulizi dhidi ya watu binafsi yakiongezeka mara tatu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Habari ID: 3480892 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/04
IQNA – Kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya misikiti nchini Uingereza na Ufaransa, viongozi wa Ulaya wametakiwa kuacha kuchochea chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3480880 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/01
IQNA – Ripoti mpya iliyotolewa Jumatatu imetoa wito kwa serikali ya Uingereza kuweka mkakati wa kitaifa wa pamoja kupambana na kuongezeka kwa cChuki Dhidi ya Uislamu (Islamophobia), ikionya kuwa mgawanyiko unaozidi katika jamii unadhoofisha imani ya wananchi kwa taasisi za umma na kutishia mshikamano wa kitaifa.
Habari ID: 3480819 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/10
IQNA – Jumuiya ya Waislamu Duniani (MWL) imekaribisha uamuzi wa mahakama ya Uingereza kumtia hatiani mtu aliyeteketeza moto nakala ya Qur’ani Tukufu mjini London.
Habari ID: 3480807 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/08
IQNA – Malalamiko ya ukiukaji wa haki za kiraia yamewasilishwa kwa Idara ya Haki za Kiraia ya Jimbo la Michigan nchini Marekani dhidi ya tawi la Domino’s Pizza lililoko Waterford, kufuatia ripoti ya ubaguzi wa kidini na uharibifu wa chakula uliowalenga wanawake wawili Waislamu na watoto wao.
Habari ID: 3480803 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/07
IQNA – Serikali ya Ufaransa imeshutumiwa kwa kulenga shirika la Ulaya linalojitolea kupambana na chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3480767 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/31
IQNA – Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) ni janga la kimataifa linaloathiri jamii nzima, si Waislamu pekee, alionya Abdulsamad Al-Yazidi, Mwenyekiti wa Kituo cha Kiislamu cha Ujerumani.
Habari ID: 3480753 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/28
IQNA – Mkutano wa kimataifa utakaofanyika Baku mnamo Mei 26–27 utawaleta pamoja wataalamu wa kimataifa ili kujadili changamoto inayoongezeka ya chuki dhidi ya Uislamu yaani Islamophobia.
Habari ID: 3480731 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/24
IQNA – Maelfu ya watu wameandamana katika mitaa ya Paris na miji mingine ya Ufaransa siku ya Jumapili kulaani ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu na kumuenzi Aboubakar Cissé, kijana kutoka Mali aliyeuawa akiswali ndani ya msikiti.
Habari ID: 3480675 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/12
IQNA-Mwanaume mmoja wa Kifaransa aliyemdunga kisu na kumuua Mwislamu aliyekuwa akisali katika msikiti ulioko kusini mwa Ufaransa, ameshtakiwa rasmi kwa mauaji ya kukusudia yanayochochewa na chuki ya kidini au kikabila, ofisi ya mwendesha mashtaka wa Nîmes ilitangaza Ijumaa.
Habari ID: 3480667 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/11
IQNA – Umoja wa Mataifa umetangaza kumteua mwanadiplomasia mkongwe wa Hispania, Miguel Angel Moratinos Cuyaubé, kuwa mjumbe maalum atakayeongoza juhudi za kushughulikia chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia), ofisi ya msemaji wa UN ilitangaza Jumatano.
Habari ID: 3480660 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/09